MCHEZAJI BORA WA WIKI NI EMMANUEL OKWI


Okwi amefikisha magoli 6 katika michezo miwili aliyoicheza mpaka sasa ya Ligi Kuu
Mshambuliaji wa Simba, raia wa Uganda, Emmanuel Okwi amefanikiwa kuibuka mchezaji bora wa wiki baada ya kuwaiwezesha klabu yake kuibuka na alama tatu muhimu, kwenye ushindi wa goli 3 kwa bila dhidi ya Mwadui.
Okwi amefanikiwa kuibuka nyota bora wa wiki baada ya kuwafunika wachezaji wengine waliokuwa na wikendi nzuri kama Peter Mapunda wa Majimaji, Katsvairo wa Singida United na wengine waliokuwa na kiwango bora.
Katika mchezo huo na Mwadui, Mganda huyo alikuwa mwiba mkali kwa safu ya ulinzi wa Mwadui,  alifanikiwa kufunga mabao mawili dakika ya ( 7, 60 ) kwa mashuti ya umbali wa mita 25 ambayo yalimshinda mlinda mlango wa wa Mwadui, Arnold Massawe.

No comments:

Post a Comment

Alichofanyiwa Rudiger na shabiki wa Chelsea

Kufatia mchezo wa jana kati ya Man city na Chelsea, Chelsea kuambilia kipigo cha goli 6, baada ya mchezo kumalizika mlinzi huyo wa kat...

Most viewed