WACHEZAJI WA REAL MADRID HAWAMTAKI ALEXIS SANCHEZ

Kwa mujibu wa habari kutoka Hispania, wachezaji wa Real Madrid wameutaka uongozi wa klabu hiyo kuachana na mpango wa kumsajili Alexis Sanchez
Imeripotiwa kuwa viongozi wa Real Madrid wamezuiliwa kufanya mchakato wa kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, kwani wachezaji wa Los Blancos wameweka bayana kuwa hawamtaki mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile Bernabeu.
Inaaminika kuwa nyota huyo wa Arsenal alikuwa kwenye rada za Los Blancos kuelekea msimu ujao wa majira ya joto, ambapo atakuwa akipatikana kama mchezaji huru.
Kwa mujibu wa chanzo cha Hispania Don Balon, hata hivyo, mchezaji huyo amekanusha kuwa hana ndoto hiyo ya kuhamia Bernabeu kwa sababu amewahi kucheza Barcelona.
Sanchez ambaye amedumu miaka mitatu Camp Nou kabla ya kujiunga na Arsenal 2014, inaaminika alikuwa akikomaa kutua aidha Madrid au Manchester City.
Imedai kuwa nahodha wa Los Blancos Sergio Ramos amekuwa mstari wa mbele kuwaambia viongozi wa Madrid kuangalia sehemu nyingine, ambako kuna wachezaji ambao Zinedine Zidane anawahitaji.

No comments:

Post a Comment

Alichofanyiwa Rudiger na shabiki wa Chelsea

Kufatia mchezo wa jana kati ya Man city na Chelsea, Chelsea kuambilia kipigo cha goli 6, baada ya mchezo kumalizika mlinzi huyo wa kat...

Most viewed