Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazili alitembea kwenda kupiga penalti waliyopata PSG dakika ya 78 mechi ya Jumapili Ligue 1 dhidi ya Lyon, timu ya Unai Emery ikiwa inaongoza kwa bao 1-0.
Lakini Edinson Cavani alikuwa ameshawahi, na mshambuliaji huyo wa Uruguay alimwambia Neymar aondoke kabla ya kurudi nyuma kupiga penalti ambayo hata hivyo iliokolewa na kipa wa Lyon Anthony Lopes.
Kwa mashindano yote hayo, hatimaye PSG waliondoka na pointi tatu ambapo amgoli kutoka kwa wachezaji hao wawili yaliwawezesha kushinda 2-0.

No comments:
Post a Comment