BALE NA MAYORAL WALIWEKA KIMIANI KUIREJESHA KWENYE NJIA ZA USHINDI RONALDO ANAPOJIANDAA KURUDI

Winga huyo raia wa Wales akiwa katika kiwango cha juu alifunga bao safi katika uwanja wa Anoeta pamoja na kinda wa Kihispania akifanya kazi nzuri pia
Gareth Bale anapenda kucheza katika uwanja wa Anoeta. Mchezaji huyo, 28, amekuwa akizomewa na mashabiki wa Real Madrid katika uwanja wa Santiago Bernabeu siku za hivi karibuni, lakini aliwapatia zawadi mahususi ugenini dhidi ya Real Sociedad. Alifanya kazi nzuri Jumapili na akishirikiana na Borja Mayoral waliirejesha Los Blancos kwenye njia za ushindi La Liga.
Kufuatia sare dhidi ya Valencia na Levante nyumbani Madrid walipoteza pointi nne kwenye mechi za La Liga hivyo kuiruhusu Barcelona kuongeza pengo la pointi dhidi yao.
Wakiwa wamepungukiwa nguvu ya mashambulizi mechi mbili zilizopita Zidane alikiri kuwa angependa kusajili mshambuliaji mwingine baada ya Alvaro Morata kuuzwa Chelsea, lakini Mfaransa huyo alimpa Mayoral nafasi ya kuanza Jumamosi pembeni ya Marco Asensio na Bale katika safu ya mashambulizi.
"Labda tunaweza kufanya vizuri tukipata namba 9 mwingine, lakini huu si mwisho," alisema wiki iliyopita. "Morata alitaka kucheza zaidi, alitaka kuondoka. Hatukuweza kuleta mchezaji mwingine, lakini namwamini [Borja] Mayoral, lakini pia tunaye Gareth. Ni kweli anacheza zaidi kama winga lakini anaweza."
Na ndivyo ilivyokuwa. Mayoral alifungua ukurasa wa mabao, akimalizia viuzri kabisa, na pia aliwalazimisha Sociedad kujiunga kipindi cha kwanza baada ya wapinzani wao kusawazisha kupitia Kevin Rodriguez, ambaye pia shuti lake lilizuiliwa na Keylor Navas.
Isco pia alicheza katika kiwango bora akipiga pasi ndefu na nzuri akimpa pande Bale, ambaye alikimbia yadi 73 na kumpita Kevin kwa kasi ya ajabu na kumfunga mlinda mlango Geronimo Rulli.
Madrid wamepata ushindi wa 11 mfululizo ugenini kwa mara ya kwanza katika historia yao na Los Blancos sasa wamefunga katika mechi zao 73 za mwisho kufikia rekodi iliyowekwa na Santos ya Pele.

No comments:

Post a Comment

Alichofanyiwa Rudiger na shabiki wa Chelsea

Kufatia mchezo wa jana kati ya Man city na Chelsea, Chelsea kuambilia kipigo cha goli 6, baada ya mchezo kumalizika mlinzi huyo wa kat...

Most viewed