Kikosi cha Arsene Wenger kimepoteza mechi zao zote za nyuma walizocheza ugenini msimu huu dhidi ya Stoke na Liverpool, lakini wangeweza kushinda pointi zote tatu Darajani, kwani Aaron Ramsey aligonga mwamba kipindi cha kwanza na goli la Shkodran Mustafi lilikataliwa kipindi cha pili.
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amedai kuwa David Luiz wa Chelsea alistahili kadi nyekundu aliyopokea katika mechi hiyo ya Ligi Kuu Uingereza Stamford Bridge.
Luiz alioneshwa kadi nyekundu katika dakika za majeruhi kwenye mechi hiyo kubwa ya London na Michael Oliver baada ya kuruka vibaya dhdi ya beki wa Arsenal Sead Kolasinac.
Ni mara ya tatu mfululizo Chelsea wamepunguzwa kucheza watu kumi dhidi ya Gunners, ambao walipata sare ya 0-0 katika uwanja wa Stamford Bridge, lakini Wenger anaamini kuwa mwamuzi alifanya maamuzi sahihi.
"Alitumia nguvu nyingi, naam. Nadhani Kolasinac hakuwa amesimama kikamilifu kwa miguu yake. Hata Luiz mwenyewe atakubali kwamba kulikuwa na umbali mkubwa na alikwenda kwa nguvu," aliwaambia waandishi.
Luiz atafungiwa mechi tatu, hii ikimaanisha ataikosa safari ya Manchester City, pamoja na mechi dhidi ya Stoke City na Crystal Palace.
Chelsea wameshindwa kufunga katika mechi yenye ushindani katika uwanja wa nyumbani chini ya Conte kwa mara ya kwanza (mechi 27).

No comments:
Post a Comment