INIESTA ASAINI MKATABA MPYA WA "MAISHA" BARCELONA AMALIZA TETESI

Mshindi wa Kombe la Dunia amejifunga kwa mkataba mpya wa maisha na miamba wa La Liga, na hataondoka kamwe Camp Nou
Andres Iniesta amezima tetesi zote zilizokuwa zikiuzingira mustakabali wake kwa kusaini mkataba mpya Barcelona.
Iniesta, 33, angekuwa mchezaji huru majira ya joto 2018, kwani mkataba wake ulikuwa unakwisha Cam Nou.
Sintofahamu ya muda mrefu iliyodumu Katalunya ilizipa klabu nyingine fursa ya kuanza kuzungumza na mchezaji huyo.
Hata hivyo Iniesta alitoa habari njema mwishoni mwa mwezi Septemba kuwa mazungumzo yalikuwa yakiendelea baina yake na klabu.
Barcelona sasa wametangaza kuwa makubaliano yamefikiwa taarifa kutoka tovuti rasmi ya klabu ikisomeka: "Andres Iniesta amesaini mkataba wa maisha na FC Barcelona Ijumaa, dili litakalomweka klabuni hapo kipindi chote cha soka lake.
"Kiungo huyo wa Hispania, ambaye amecheza mechi 639 Barca, ni mchezaji wa pili kucheza mechi nyingi wa muda wote klabuni hapo.
"Amefunga magoli 55 kwenye timu ya kwanza, tangu alipoanza kucheza Oktoba 29, 2002.
"Tangu 2015 Iniesta amekuwa nahodha wa kikosi cha kwanza na ni miongoni mwa wachezaji ambao ni kama nembo ya klabu.
"Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 33 alijiunga na klabu Septemba 1996, akiwa na miaka 12.
"Iniesta na Leo Messi wana rekodi moja ya kutwaa mataji mengi zaidi katika historia ya Barce, 30."
Habari zaidi inafuata...

No comments:

Post a Comment

Alichofanyiwa Rudiger na shabiki wa Chelsea

Kufatia mchezo wa jana kati ya Man city na Chelsea, Chelsea kuambilia kipigo cha goli 6, baada ya mchezo kumalizika mlinzi huyo wa kat...

Most viewed