Lionel Messi alipata hat-trick na Ousmane Dembélé alikuwa na mwanzo wa mafanikio katika klabu hiyo, na Barca walionekana kuwa thabiti kuelekea mechi ya ufunguzi Ligi ya Mabingwa dhidi ya Juventus.
Ousmane Dembélé atafanya mambo makubwa
Licha ya mwanzo mzuri na kutoa pasi ya goli, bado haimpi uhakika wa kuwa mchezaji bora zaidi wa klabu katika historia, lakini Mfaransa huyo ameonyesha ishara njema ya kuisaidia Barca. Dembélé ameonyesha uwezo katika kila kitu, kasi, weledi, pasi, akili, kila kitu. Hakuwa mchezaji aliyekosa utulivu, na umakini wake ulikuwa mzuri sana katika mechi yake ya kwanza nyumbani.
Dembélé huenda akaanzia benchi dhidi ya Juventus kwani bado Valverde angali akimsaidia kuzoea mfumo, lakini hakuna shaka, atafanya maajabu katika mechi ya Jumanne na zaidi. Dembélé atakuwa miongoni mwa magwiji wa Blaugrana, hakuna swali.

No comments:
Post a Comment