JOSE MOURINHO AKIRI STOKE CITY WALISTAHILI POINTI

ndondo2017.blogspot.com
Jose Mourinho amedai kuwa wachezaji wake walicheza katika kiwango cha kawaida sana, lakini pointi ni pointi.
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amekiri kuwa matokeo ya sare yalikuwa ya haki timu yake ilipopamba dhidi ya Stoke City Ligi Kuu Uingereza Jumamosi.
Mashetani Wekundu walishuhudia mwanzo wao mzuri kwa ushindi asilimia 100 ukikoma ugenini dhidi ya Stoke City, Eric Maxim Choupo-Moting akifunga mara mbili kufuta mabao ya marcus Rashford na Romelu Lukaku.
Mourinho amedai kuwa mapumziko ya mechi za kimataifa yamekuwa na athari katika ufanisi wa kikosi chake, lakini bado anaamini United walikuwa karibu kushinda mechi hiyo kuliko kupoteza.
"Ilikuwa mechi ngumu kwa sababu tofauti-tofauti. Wachezaji wangu, baada ya mapumziko ya kimataifa si wale wa siku zote," alisema Mourinho.
"Walicheza katika kiwango cha kawaida lakini tulikuwa mchezoni, tulipambana na tulikaribia kushinda kuliko hata kufunga.
"Stoke ni wakubwa, shupavu na wana nguvu kwenye mipira ya juu. Walipambana kwa nguvu, na nadhani walistahili pointi. Pointi ni pointi. Sicho tulichokijia lakini pointi ni pointi."
Mourinho pia alikiambia BBC Sport: "Hapana sijafurahishwa na ile pointi kwa sababu tulikuwa karibu kushinda. Lakini naweza kusema ni matokeo ninayoyakubali.
United sasa wanageuzia macho yao kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa, ambapo wataikaribisha Basel Jumanne.

No comments:

Post a Comment

Alichofanyiwa Rudiger na shabiki wa Chelsea

Kufatia mchezo wa jana kati ya Man city na Chelsea, Chelsea kuambilia kipigo cha goli 6, baada ya mchezo kumalizika mlinzi huyo wa kat...

Most viewed