Mshambuliaji chipukizi wa Tanzania, Yohana Oscar Mkomola amefuzu majaribio katika klabu ya Esperance inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Tunisia.
Akizungumza na mtandao wa Zubeiry sports online, Mkomola amesema kila kitu kimeenda vizuri na anacho subiri ni kusaini mkataba na klabu hiyo kwa sasa
Katika hatua nyingine Mkomola amesema atatakiwa kuchezea timu ya vijana hadi April mwakani atakapofikisha umri wa miaka 18 ndipo asaini mkataba na kuanza kuchezea timu ya wakubwa.
“Nimerudi hapa nyumbani kukamilisha taratibu fulani, baada ya wiki mbili nitaondoka kurejea Tunisia ambako nikifika kwanza nitaanza kuchezea timu B ya vijana hadi nifikishe umri wa miaka 18 mwezi wa nne (2018) ndipo nisaini mkataba na kuanza kuchezea timu ya wakubwa,”amesema

No comments:
Post a Comment