Beki wa kulia wa Yanga Hassani Ramadhani ‘Kessy’ amemtaka kocha wake George Lwandamina kumwamini na kumpa nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza.
Kessy licha ya kusajiliwa kwa mbwebwe akitokea kwa mahasimu wao Simba, amekuwa akisota benchi kuwania namba ya kucheza kikosi cha kwanza mbele ya Juma Abduli.
Kessy,licha ya kuwa fiti lakini changamoto anayokutana nayo msimu huu ni kucho wake Lwandamina kutokuwa na imani naye kwa kumweka benchi.
“Nipo kwenye kiwango bora hivi sasa lakini changomto ninayokutana nayo ni kocha kuniamini, ingawa hivyo nivitu vya kawaida naamini ipo siku nitapewa nafasi na kuonyesha kiwango changu,”amesema Kessy.
Beki huyo amesema ataendelea kufanya mazoezi kwa bidii ili kumshawishi kocha wake, Lwandamina aweze kumpa nafasi kama ambavyo anataka.
Kessy amesema tangu atue Yanga hajapata nafasi ya kutosha kuonyesha uwezo wake halisi ambao amekuwa akionyesha akiwa Mtibwa Sugar na timu nyingine alizopitia.
Beki huyo amekuwa akisota benchi kwa muda mrefu huku akipewa nafasi ndogo ya kucheza na kocha huyo raia wa Zambia, ambaye amemkuta kwenye kikosi cha Yanga.

No comments:
Post a Comment