Klabu hiyo ya La Liga ilitangaza Julai kuwa Messi amekubali mkataba mpya wa miaka minne na ilikuwa mkataba usaini baada ya wiki chache Messi atakaporudi kutoka kwenye maandalizi ya msimu.
Tangu hapo hapakuwa na tamko rasmi na tetesi ziliendelea kusambaa kuhusu mustakabali wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30.
Bartomeu, sasa, amezungumza kupitia televisheni ya Catalan kuthibitisha kuwa mshindi huyo wa mara tano wa Ballon d'Or Messi amejifunga Nou Camp kwa mkataba mpya.

No comments:
Post a Comment