LIVERPOOL ITAWEZA KUPINDUA MBELE YA LEICESTER CITY KING POWER?


Leicester wameifunga Liverpool katika mechi tatu za mwisho walizokutana King Power - mechi ya mwisho kabisa ikiwa Kombe la EFL Jumanne usiku
Liverpool wanataka kukomesha mwendo wa mechi nne bila ushidi katika michuano yote watakaposafiri kwenda Leicester City kwenye Ligi Kuu Uingereza Jumamosi mchana.
Mechi hiyo inakuja tena ikiwa ni siku nne tu tangu timu hizo zikutane kwenye mechi ya Kombe la EFL, Leicester wakiibuka na ushindi wa 2-0 katika ardhi ya nyumbani kwao na kutinga raundi ya 16.
Haipingiki kwamba Leicester walikuwa kwenye wakati mgumu kupata matokeo katika hatua za mwanzo kampeni za 2017-18, lakini Foxes wamekumbana na mechi ngumu sana.
Walichezea kichapo cha 4-3 dhdi ya Arsenal katika mechi ya ufunguzi wa msimu, lakini walirejea kwenye njia za ushindi baada ya kushinda 2-0 dhidi ya Brighton & Hove Albion.
Foxes walipoteza mchezo dhidi ya Manchester United na dhidi ya Chelsea kwenye uwanja wa nyumbani, kabla ya kupata sare ya 1-1 Huddersfield Town wikiendi iliyopita. Jumla ya pointi nne tu kutoka kwenye mechi tano, na wanashika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi.
Lakini jambo la kuogopesha ni kwamba Leicester wamecheza mechi moja tu bila kuruhusu goli na wameruhusu magoli 18 katika mechi nane za mwisho Ligi Kuu Uingereza, na ikiwa watapoteza mechi wikiendi hii watafikia idadi ya pointi ndogo zaidi walizowahi kupata katika mechi sita Uingereza.

Vijana wa Shakespeare wataingia dimbani wakiwa na ari wakitaka kuonyesha kuwa ushindi wa 2-0 waliopata dhidi ya Liverpool kwenye Kombe la EFL haukuwa wa kubahatisha.
Liverpool wamejikusanyia pointi saba kutoka kwenye mechi tatu za mwanzo katika msimu wa Ligi Kuu Uingereza wa 2017-18, na mambo yalikuwa murua pale waliposhinda mabao 4-0 dhidi ya Arsenal Agosti 27.
Tangia hapo, kikosi cha Jurgen Klopp kimeshindwa kupata ushindi katika mechi nne kwenye michuano mitatu tofauti. Reds walinyukwa 5-0 Manchester City baada ya mapumziko, kabla ya kupata sare dhidi ya Sevilla na Burnley kwenye Ligi ya Mabingwa na Ligi ya Uingereza mtawalia.
Liverpool imeshinda pointi 132 katika mechi 73 chini ya Klopp, ambazo ni pointi tisa pungufu katika kipindi sawa chini ya Brendan Rodgers ambaye alitupiwa virago kama kocha mkuu Oktoba 2015.

No comments:

Post a Comment

Alichofanyiwa Rudiger na shabiki wa Chelsea

Kufatia mchezo wa jana kati ya Man city na Chelsea, Chelsea kuambilia kipigo cha goli 6, baada ya mchezo kumalizika mlinzi huyo wa kat...

Most viewed