Manchester United walipata ushindi kwenye Kombe la Carabao Jumatano, Marcus Rashford akifunga mabao mawili ya mapema na kutoa pasi moja ya goli wakiitungua 4-0 Burton Albion katika uwanja wa Old Trafford.
Kinda huyo sasa ameifungia United mabao 24 na bado hajatimiza miaka 20, kiwango chake cha msimu huu ni ishara kuwa amepevuka.
Hata Wayne Rooney hakuweza kufunga mabao mengi kwa klabu akiwa na umri wa Rashford, na nahodha huyo wa zamani wa Uingereza aliweka rekodi ya magoli 253 kabla ya kurejea Everton majira ya joto.
Awali, alitabiriwa na Jose Mourinho kuwa ataikaribia rekodi ya Rooney, Rashford ameendelea kuwa mshambuliaji mahiri.
Na mwandishi wa Manchester United Kris Voakes anasema, ikiwa bado n siku za mapema sana kwa Rashford, ameonesha dalili zote za kuwa shujaa wa United sambamba na magwiji wa miaka iliyopita.

No comments:
Post a Comment