NYOTA BORA WA WIKI

Yakubu Mohammed alikuwa kikwazo kwa upande wa Simba kushindwa kuondoka na alama tatu
Mlinzi wa kati wa klabu ya Azam, Yakubu Mohammed amefanikiwa kuwa mchezaji bora wa wiki baada ya kuwa katika kiwango bora kwenye mechi dhidi ya Simba.
Azam na Simba waligawana pointi kwenye mchezo uliomalizika  kwa sare ya bila kufungana siku ya Jumamosi kwenye uwanja wa Chamanzi.
Yakubu Mohammed ameibuka nyota wa wiki baada ya kuwazidi wachezaji kadhaa waliokuwa na wikendi nzuri kama James Kotei, Ibrahim Ajibu, Marcel Kaheza na wengineyo.
Yakubu alikuwa kikwazo kwa upande wa Simba  kushindwa kuibuka na alama tatu licha ya kusheheni nyota wenye uwezo mkubwa, Yakubu alifanikiwa kuziba mianya yote hatari, alikuwa bora kwa mipira ya juu na ya chini mbele ya mastraika wa Simba John Bocco na washambuliaji wengine wa Mnyama.
Katika hatua nyingine pia Mghana huyo alikuwa bora kwenye matumizi ya nguvu hasa kwenye mipira ile ya kugombea dhidi ya wapinzani wake siku hiyo.

No comments:

Post a Comment

Alichofanyiwa Rudiger na shabiki wa Chelsea

Kufatia mchezo wa jana kati ya Man city na Chelsea, Chelsea kuambilia kipigo cha goli 6, baada ya mchezo kumalizika mlinzi huyo wa kat...

Most viewed