![]() |
| ndondo2017.blogspot.com |
Lionel Messi alitikisa nyavu mara mbili Barcelona ikitoka kifua mbele kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Juventus mechi ya kwanza Ligi ya Mabingwa msimu wa 2017-18, kadhalika Paris Saint-Germain, Manchester United na Chelsea zilipata ushindi mnono Jumanne.
Baada ya msimu wa majira ya joto uliojaa adha tele, Barca walikabiliana na mshindi wa pili wa michuano hiyo msimu uliopita, huenda hawakucheza katika kiwango walichotaka kama timu, lakini Lionel Messi alidhihirisha umahiri wake akiiwezesha Blaugrana kushinda pointi tatu muhimu.
Mchezaji mpya Ousmane Dembele alipewa nafasi kikosi cha kwanza Camp Nou, lakini ni Messi aliyeweka kimiani bao la kufungua ukurasa baada ya kugongeana vema kabisa na Luis Suarez.

No comments:
Post a Comment