![]() |
| ndondo2017.blogspot.com |
"Namhitaji." Hayo yalikuwa maneno ya Jose Mourinho kuhusu Marouane Fellaini kabla ya mechi ya Manchester United Ligi ya Mabingwa dhidi ya Basel Jumanne.
Haikumchukua muda mrefu kiungo huyo kuonesha ni kwa nini anahitajika, akiingia kutokea benchi baada ya Paul Pogba kupata majeraha dakika ya 18 ya mchezo aliipatia bao la kwanza United iliyoshinda 3-0 Old Trafford.
Fellaini alionesha vitu vingi zaidi ya goli alilofunga. Alimsaidia Nemanja Matic alipopoteza mpira katika mazingira ya hatari, lakini pia alipiga krosi maridadi kwa Marcus Rashford aliyefunga ukurasa wa mabao dhidi ya Basel.

No comments:
Post a Comment