MANCHESTER UNITED KUELEKEA MCHEZO DHIDI YA EVERTON

Jose Mourhino amethibitisha kiungo wa Manchester United, Paul Pogba atahukosa mchezo wa Jumapili dhidi ya Everton kutokana na kuuguza majeraha
kiungo Mfaransa alichaguliwa kuwa kapteni kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya FC Basel, lakini alitolewa kwenye kipindi cha kwanza kutokana na tatizo la misuli. Nafasi yake ilichukuliwa na Maroune Fellaini na Mbelgiji huyo alionesha thamani yake, alifunga goli  na kusaidia lingine la Marcus Rashford.
Akizungumza na MUTV wakati wa mahojiano katika Complex Aon Training,Jose alianza kwa kutoa taarifa juu ya afya ya Pogba. "Ni mejeruhi na hawezi kucheza siku ya Jumapili," meneja alituambia.
Mourihno amesema hajui kwa muda gani Pogba atakuwa nje na baadaye aliongeza: "Tunajua kwamba, kwa mechi chache, sijui ngapi, lakini natarajia tutacheza bila Pogba kwa mechi chache "Hata hivyo, Jose alikuwa na nia ya kusisitiza kutokuwepo kwake ni fursa nzuri kwa kikosi kimoja kupambana.

No comments:

Post a Comment

Alichofanyiwa Rudiger na shabiki wa Chelsea

Kufatia mchezo wa jana kati ya Man city na Chelsea, Chelsea kuambilia kipigo cha goli 6, baada ya mchezo kumalizika mlinzi huyo wa kat...

Most viewed