CONTE: N'GOLO KANTE NI MCHEZAJI MWENYE UWEZO MKUBWA

ndondo2017.blogspot.com

N'Golo Kante amekuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Chelsea, na Conte amekiri kuwa mchezaji huyo anaimarika kila kukicha
Meneja wa Chelsea Antonio Conte amedai kuwa N'Golo Kante amethibitisha kuwa yeye ni mchezaji bora wa anga nyingine wiki za kwanza katika Ligi Kuu Uingereza.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa alikuwa mchezaji bora wa mwaka wa tuzo za PFA 2016-17 baada ya kuisaidia Chelsea kupata mafanikio, miezi 12 tu baada ya kufanya hivyo akiwa Leicester City.
Kante aling'ara kwa mara nyingine mabingwa hao watetezi wakishinda 2-1 dhidi ya Leicester katika uwanja wa King Power, Conte hakuweza kuficha furaha yake kuhusu nyota huyo.
"N'Golo ni mchezaji muhimu sana kwetu - mchezaji mkubwa," aliwaambia waandishi. "Kilikuwa ni kiwango cha kuvutia. Alicheza soka safi sana. Alifunga lakini bado alifanya kazi kubwa sana. Kila siku anaimarika. Nadhani anakuwa bora zaidi akiwa na mpira.
"Hapo mwanzo, watu wengi waliniambia, 'Ni mchezaji mzuri bila ya mpira, ana stamina na mchapakazi', lakini sasa ni mzuri akiwa na mpira pia."
Chelsea ambao wameshinda mechi tatu mfululizo na kupanda hadi nafasi ya tatu msimamo wa Ligi ya Uingereza, watashuka dimbani tena wiki hii kuikabili Qarabag kwenye Ligi ya Mabingwa.

No comments:

Post a Comment

Alichofanyiwa Rudiger na shabiki wa Chelsea

Kufatia mchezo wa jana kati ya Man city na Chelsea, Chelsea kuambilia kipigo cha goli 6, baada ya mchezo kumalizika mlinzi huyo wa kat...

Most viewed