NEMANJA MATIC ASEMA MOURINHO NI KOCHA BORA ZAIDI ALIYEFANYA NAYE KAZI

Nemanja Matic amesema bosi wa Manchester United Jose Mourinho ndiye kocha bora zaidi aliyewahi kufanya naye kazi
Mserbia huyo alitamka kuwa uwepo wa Mourinho Man United ndio uliomfanya aamue kutua Old Trafford majira ya joto.
"Mourinho ni mtu wa kipekee, na kocha bora niliyewahi kufanya naye kazi," kiungo huyo mkabaji alisema. "Wakati mwingine si rahisi kufanya naye kazi, kwa sababu anahitaji kazi zaidi.
"Hata unapocheza katika kiwango cha juu zaidi katika mechi, anakutaka ucheze zaidi mechi inayofuata."
Matic anaendelea vizuri chini ya Mourinho baada ya kutua United kwa paundi milioni 35, na ameendeleza ubora wake katika safu ya kiungo United wakiifunga Benfica 1-0 Ligi ya Mabingwa Jumatano.
Wawili hao walitwaa taji Ligi Kuu Uingereza miaka miwili iliyopita wakiwa Chelsea na Matic bado anamsifia meneja wake.
"Kiuhalisia ni mtu tofauti kabisa na anavyochukuliwa na umma wote," alisema. "Ni mtu mwenye sifa zote za kibinadamu. Si mtu yule anayezungumziwa tofauti kwenye vyombo vya habari.
"Ameunda kundi bora la wachezaji wenye uwezo, na tunakila kitu cha kutuwezesha kupata matokeo mazuri."

OSCAR AMESEMA BADO ANA MATUMAINI YA KUREJEA CHELSEA KWA SIKU ZA BAADAYE

Kiungo wa Brazil, Oscar amesema kuwa anataka kurudi Ligi ya Uingereza kabla ya kufikisha umri wa miaka 30 na ana matumaini ya kujiunga tena na Chelsea
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 aliondoka Stamford Bridge kwa dau kubwa la fedha kwenda Ligi Kuu la China mwezi Januari, aliigharimu klabu ya Shanghai SIPG paundi millioni 60 kuinasa saini yake.
Oscar amekuwa na fomu nzuri kwa sasa, akiwa sehemu ya kikosi cha kwanza amefaniki kufunga mabao tisa katika mechi 17 kwa Red Eagles, lakini tayari ameshaanza kuifikiria kurejea klabu yake ya zamani Chelsea zaidi chini ya mstari.

"Ndiyo, nitarejea. Mimi bado ni mdogo, nina umri wa miaka 26," aliiambia Premier League Brasil. "Ni nani anayejua, katika miaka miwili au mitatu kurudi Ligi Kuu ya Uingereza ... Nitakuwa na furaha sana.Na hasa kwa Chelsea, ambayo imenifungulia milango ya kurudi."

MOURINHO: "MAN UNITED HAIJAFANYA CHOCHOTE"

Mourinho amekiri kuwa timu yake imeanza vizuri, lakini amesisitiza kuwa bado kuna kazi kubwa dhidi ya mahasimu wakuu
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amesema kuwa timu yake haijafanya chochote katika mbio za taji Ligi Kuu Uingereza.
United wameshinda mara sita na sare moja katika mechi zao saba za msimu huu, ingawa bado hawajakabiliana na wapinzania wanaoaminika kuwa washindani halisi wa taji.
Mourinho amekiri kuwa timu yake imeanza vizuri, lakini amesisitiza kuwa bado kuna kazi kubwa mbeleni ikiwa klabu hiyo inataka kuendelea kubaki kileleni.

DARMIAN: "DAVID DE GEA NI KIPA BORA KULIKO GIANLUIGI BUFFON"

Darmian anaamini Buffon, 39, ni kipa bora wa muda wote, lakini beki huyo anahisi De Gea ndiye mwenye kiwango safi kwa sasa
Beki wa Manchester United Matteo Darmian amebainisha kuwa anamchukulia David de Gea kama kipa bora duniani, mbele ya Muitaliano mwenzake Gianluigi Buffon.
De Gea amefurahia mwanzo mzuri msimu huu, akicheza mechi saba bila kuruhusu goli baada ya kucheza mechi tisa Ligi Kuu Uingereza na Ligi ya Mabingwa, wakati Buffon akiendeleza umahiri Juventus.
Darmian anaamini Buffon, 39, ni kipa bora wa muda wote, lakini beki huyo anahisi De Gea ndiye mwenye kiwango safi kwa sasa.

INIESTA ASAINI MKATABA MPYA WA "MAISHA" BARCELONA AMALIZA TETESI

Mshindi wa Kombe la Dunia amejifunga kwa mkataba mpya wa maisha na miamba wa La Liga, na hataondoka kamwe Camp Nou
Andres Iniesta amezima tetesi zote zilizokuwa zikiuzingira mustakabali wake kwa kusaini mkataba mpya Barcelona.
Iniesta, 33, angekuwa mchezaji huru majira ya joto 2018, kwani mkataba wake ulikuwa unakwisha Cam Nou.
Sintofahamu ya muda mrefu iliyodumu Katalunya ilizipa klabu nyingine fursa ya kuanza kuzungumza na mchezaji huyo.
Hata hivyo Iniesta alitoa habari njema mwishoni mwa mwezi Septemba kuwa mazungumzo yalikuwa yakiendelea baina yake na klabu.
Barcelona sasa wametangaza kuwa makubaliano yamefikiwa taarifa kutoka tovuti rasmi ya klabu ikisomeka: "Andres Iniesta amesaini mkataba wa maisha na FC Barcelona Ijumaa, dili litakalomweka klabuni hapo kipindi chote cha soka lake.
"Kiungo huyo wa Hispania, ambaye amecheza mechi 639 Barca, ni mchezaji wa pili kucheza mechi nyingi wa muda wote klabuni hapo.
"Amefunga magoli 55 kwenye timu ya kwanza, tangu alipoanza kucheza Oktoba 29, 2002.
"Tangu 2015 Iniesta amekuwa nahodha wa kikosi cha kwanza na ni miongoni mwa wachezaji ambao ni kama nembo ya klabu.
"Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 33 alijiunga na klabu Septemba 1996, akiwa na miaka 12.
"Iniesta na Leo Messi wana rekodi moja ya kutwaa mataji mengi zaidi katika historia ya Barce, 30."
Habari zaidi inafuata...

INIESTA: "BARCELONA HAIWEZI KUISHI BILA LIONEL MESSI"

Josep Maria Bartomeu amesisitiza mara kadhaa kuwa ni swala la muda tu tangazo litatolewa, lakini Iniesta anataka tetesi zikome mara moja
Andres Iniesta amewataka viongozi wa Barcelona kuhakikisha Lionel Messi anasaini mkataba mpya kwani klabu "haiwezi kuishi bila yeye".
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina bado hajajifunga rasmi na miamba wa Catalan, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kufika tamati mwishoni mwa msimu.
Rais wa Barca Josep Maria Bartomeu amesisitiza mara kadhaa kuwa ni swala la muda tu tangazo litatolewa, lakini Iniesta - ambaye binafsi amesaini Ijumaa mchana anataka tetesi zikome kabisa.
"Kwa swala la Leo nadhani hakuna shida katika swala la mazungumzo," aliwaambia waandishi. "Klabu inamhitaji Leo, anahitaji kuwa hapa. Natumai habari zake [katika Barca] hazitakoma.
"Ni wa kipekee, hatuwezi kuishi bila yeye na nadhani klabu inafikiri namna hiyo hiyo. Ni swala la muda tu, lakini natumai atasaini mkataba mpya mapema iwezekanavyo."
Iniesta amefuta shaka zote juu ya mustakabali wake Barcelona baada ya kukubali kusaini mkataba wa "maisha" Camp Nou.

Alichofanyiwa Rudiger na shabiki wa Chelsea

Kufatia mchezo wa jana kati ya Man city na Chelsea, Chelsea kuambilia kipigo cha goli 6, baada ya mchezo kumalizika mlinzi huyo wa kat...

Most viewed