Alichofanyiwa Rudiger na shabiki wa Chelsea



Kufatia mchezo wa jana kati ya Man city na Chelsea, Chelsea kuambilia kipigo cha goli 6, baada ya mchezo kumalizika mlinzi huyo wa kati wa timu Chelsea na ujerumani aliamua kuvua jezi yake na kugawa kwa shabiki kama ishara ya kuomba radhi ila shabiki kutokana na uchungu wa kipigo hicho aliamua kumrushia ticket kuashiria kutofurahishwa na matokeo hayo

Man city 6-0 Chelsea

Ole Gunnar Solskjaer aweka wazi Maagizo aliyopewa


Ole Gunnar Solskjaer amebainisha kuwa alikuwa na kazi ya kuinua Manchester United baada ya kuteuliwa kuwa msimamizi wa muda.

Kocha mwenye asili ya Norway  aliteuliwa kama meneja wa muda wa klabu mwezi  Desemba kufuatia kufukuzwa kwa Jose Mourinho.

Tangu Solskjaer ameingia amefanya  mabadiliko makubwa ya kihisia huko Old Trafford ambayo yamefanya Man utd kutopoteza  mechi 10 na kufanya man Utd kutimiza ndoto zao za kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa.

Ushindi dhidi ya Fulham katika Ligi Kuu ya Jumamosi umeifanya man Utd kuingia katika nafasi 4 bora za ligi hiyo

Akizungumza kocha huyo mwenyewe umri wa miaka 45 aliweka bayana maelezo aliyopewa alipokabidhiwa timu hiyo

Akiizungumza na sky sports  maelezo aliyopewa  "Manchester United iwe timu pendwa na kila aliye kwenye timu afurahie kuwepo kwenye timu na kuipenda timu"

Man United kutoa €80 milion kwa Tanguy Ndombele



Manchester United imefanya mawasiliano na kuonyesha nia ya kumsajili Tanguy Ndombele katika dirisha la uhamisho wa majira ya joto, kulingana na tetesi za usajiri .
Le10 Sport ya nchini Ufarasa imeripoti kuwa Man City na United wako kwenye ushindani  kumsajili kiungo huyo wa Lyon na ufaransa mwenye umri wa miaka 22.
Man city waliamua  Ndombele anapaswa kuhamia mwishoni mwa msimu, hata hivyo sasa United imeongeza jitihada zao juu ya mpango huo.
Ripoti hiyo inaonyesha United  amefanya kuwasiliana na wakala  wa wachezaji,  juu ya uhamisho wa kiungo wa Ufaransa mwishoni mwa msimu huu.
Kwa mujibu wa ripoti ya United na City, wote wawili walitakiawa katoa ada € 80millioni, ili kupata sgining yake.
Hata hivyo, report hiyo imesema kwamba Juventus pia wameonyesha nia ya kumtaka Ndombele  kwa njia yoyote kwa kupiku vilabu vya Manchester.


NEMANJA MATIC ASEMA MOURINHO NI KOCHA BORA ZAIDI ALIYEFANYA NAYE KAZI

Nemanja Matic amesema bosi wa Manchester United Jose Mourinho ndiye kocha bora zaidi aliyewahi kufanya naye kazi
Mserbia huyo alitamka kuwa uwepo wa Mourinho Man United ndio uliomfanya aamue kutua Old Trafford majira ya joto.
"Mourinho ni mtu wa kipekee, na kocha bora niliyewahi kufanya naye kazi," kiungo huyo mkabaji alisema. "Wakati mwingine si rahisi kufanya naye kazi, kwa sababu anahitaji kazi zaidi.
"Hata unapocheza katika kiwango cha juu zaidi katika mechi, anakutaka ucheze zaidi mechi inayofuata."
Matic anaendelea vizuri chini ya Mourinho baada ya kutua United kwa paundi milioni 35, na ameendeleza ubora wake katika safu ya kiungo United wakiifunga Benfica 1-0 Ligi ya Mabingwa Jumatano.
Wawili hao walitwaa taji Ligi Kuu Uingereza miaka miwili iliyopita wakiwa Chelsea na Matic bado anamsifia meneja wake.
"Kiuhalisia ni mtu tofauti kabisa na anavyochukuliwa na umma wote," alisema. "Ni mtu mwenye sifa zote za kibinadamu. Si mtu yule anayezungumziwa tofauti kwenye vyombo vya habari.
"Ameunda kundi bora la wachezaji wenye uwezo, na tunakila kitu cha kutuwezesha kupata matokeo mazuri."

OSCAR AMESEMA BADO ANA MATUMAINI YA KUREJEA CHELSEA KWA SIKU ZA BAADAYE

Kiungo wa Brazil, Oscar amesema kuwa anataka kurudi Ligi ya Uingereza kabla ya kufikisha umri wa miaka 30 na ana matumaini ya kujiunga tena na Chelsea
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 aliondoka Stamford Bridge kwa dau kubwa la fedha kwenda Ligi Kuu la China mwezi Januari, aliigharimu klabu ya Shanghai SIPG paundi millioni 60 kuinasa saini yake.
Oscar amekuwa na fomu nzuri kwa sasa, akiwa sehemu ya kikosi cha kwanza amefaniki kufunga mabao tisa katika mechi 17 kwa Red Eagles, lakini tayari ameshaanza kuifikiria kurejea klabu yake ya zamani Chelsea zaidi chini ya mstari.

"Ndiyo, nitarejea. Mimi bado ni mdogo, nina umri wa miaka 26," aliiambia Premier League Brasil. "Ni nani anayejua, katika miaka miwili au mitatu kurudi Ligi Kuu ya Uingereza ... Nitakuwa na furaha sana.Na hasa kwa Chelsea, ambayo imenifungulia milango ya kurudi."

MOURINHO: "MAN UNITED HAIJAFANYA CHOCHOTE"

Mourinho amekiri kuwa timu yake imeanza vizuri, lakini amesisitiza kuwa bado kuna kazi kubwa dhidi ya mahasimu wakuu
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amesema kuwa timu yake haijafanya chochote katika mbio za taji Ligi Kuu Uingereza.
United wameshinda mara sita na sare moja katika mechi zao saba za msimu huu, ingawa bado hawajakabiliana na wapinzania wanaoaminika kuwa washindani halisi wa taji.
Mourinho amekiri kuwa timu yake imeanza vizuri, lakini amesisitiza kuwa bado kuna kazi kubwa mbeleni ikiwa klabu hiyo inataka kuendelea kubaki kileleni.

DARMIAN: "DAVID DE GEA NI KIPA BORA KULIKO GIANLUIGI BUFFON"

Darmian anaamini Buffon, 39, ni kipa bora wa muda wote, lakini beki huyo anahisi De Gea ndiye mwenye kiwango safi kwa sasa
Beki wa Manchester United Matteo Darmian amebainisha kuwa anamchukulia David de Gea kama kipa bora duniani, mbele ya Muitaliano mwenzake Gianluigi Buffon.
De Gea amefurahia mwanzo mzuri msimu huu, akicheza mechi saba bila kuruhusu goli baada ya kucheza mechi tisa Ligi Kuu Uingereza na Ligi ya Mabingwa, wakati Buffon akiendeleza umahiri Juventus.
Darmian anaamini Buffon, 39, ni kipa bora wa muda wote, lakini beki huyo anahisi De Gea ndiye mwenye kiwango safi kwa sasa.

Alichofanyiwa Rudiger na shabiki wa Chelsea

Kufatia mchezo wa jana kati ya Man city na Chelsea, Chelsea kuambilia kipigo cha goli 6, baada ya mchezo kumalizika mlinzi huyo wa kat...

Most viewed